MDAU: ULIPAJI WA MAHARI UNASHUSHA UTU, HAINA TOFAUTI NA BIASHARA YA UTUMWA - Anasema kigezo cha Mahari kuwa Utamaduni ni kitu kinachovunja Utu wa Mtu kwa kuwa Mtu hawezi kuthaminishwa kwa kiwango chochote kile cha Fedha au Mali - Anadai Wazazi na Walezi wanawafanyia tathmini Watoto wao kutokana na Tabia, Uzuri, Rangi, Maumbile, Elimu. Ajabu unakuta Mzazi anasema hauwezi kuoa Mwanangu bila Tsh. Milioni 5 au 10 au bila Ng'ombe 10 - Anashauri ni vema Wazazi wa pande zote wachange Fedha kisha wawape wanaofunga Ndoa kama kianzio cha Maisha. - #Maisha #HumanRights #JamiiForums
December 04, 2022
KENYA: RUTO, RAILA WATUPIANA MANENO KUHUSU MAKAMISHNA WA UCHAGUZI WALIOSIMAMISHWA KAZI - Rais #WilliamRuto amemtaka Kiongozi wa Azimio la Umoja, #RailaOdinga kuacha kushawishi Umma kupinga maamuzi hayo kwa kuwa Mahakama ndio itaamua kuhusu Makamishna waliopinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2022 - Raila ameandika kupitia #Twitter akimjibu Ruto kwa kuweka kipande cha video kikimuonesha Ruto akipinga matokeo ya Urais Mwaka 2007 wakati Mwai Kibaki alipotangazwa kushinda na kuandika “Usijifanye leo hii kwamba umesahau.” - #Democracy #Accountability #KenyaDecides2022 #JamiiForums
December 04, 2022
BURKINA FASO: JESHI LAKIFUNGIA KITUO CHA REDIO RFI YA UFARANSA - Serikali ya Kijeshi imechukua maamuzi hayo ikidai Kituo hicho kimetangaza taarifa za Uongo na kuwapa nafasi Waasi kusikika kwenye matangazo yao - Pia, Jeshi limesema RFI ilirudia ripoti iliyokanushwa kwamba Rais Kapteni Ibrahim Traore aliyeingia Madarakani kwa Mapinduzi ya Kijeshi alisema kuna jaribio la Mapinduzi ya kumng'oa Madarakani - RFI imesema inasikitishwa na uamuzi huo na kwamba agizo la kusitisha matangazo limetolewa bila onyo na bila kufuatwa taratibu zilizowekwa na Mamlaka za Udhibiti wa Mawasiliano. - #JamiiForums #Democracy #PressFreedom #SocialJustice
December 04, 2022
AFRIKA KUSINI: RAIS RAMAPHOSA HATAJIUZULU KUTOKANA NA KASHFA INAYOMKABILI - Rais wa Afrika Kusini #CyrilRamaphosa hatajiuzulu kutokana ya kashfa ya Fedha zilizofichwa Shambani kwake licha ya Wataalamu wa Sheria kuhitimisha kuwa ana kesi ya kujibu - Kashfa hiyo ilizuka Juni, 2022, baada ya Mkuu wa zamani wa Ujasusi, Arthur Fraser, kuwasilisha malalamiko kwa Polisi akimshtumu Rais kwa Wizi wa zaidi ya Tsh. Bilioni 9 zilizokuwa katika Shamba lake la #PhalaPhala Mwaka 2020. - Hata hivyo, Msemaji wa Rais amesema Rais atapambana, na badala ya kujiuzulu atawania muhula wa pili kama Kiongozi wa Chama chake cha African National Congress (ANC) - #JamiiForums #Accountability #Democracy #Governance
December 04, 2022
#FIFAWORLDCUP2022: ARGENTINA YAIFUATA UHOLANZI ROBO FAINALI - Akicheza mechi yake ya 1,000 tangu aanze kucheza soka, Lionel Messi amefunga goli lake la 9 katika michuano yote ya Kombe la Dunia akimzidi Diego Maradona kwa upande wa timu ya taifa ya #Argentina - Messi amefikisha rekodi hiyo wakati Argentina ikiifunga Australia magoli 2-1 na kuingia Robo Fainali ambapo timu hiyo itakipiga dhidi ya Uholanzi katika Robo Fainali - Gabriel Batistuta ndiye anayeshika rekodi ya kufunga magoli mengi katika michuano hiyo akiwa amefunga magoli 10 kwa upande wa Argentina - #Qatar2022 #FIFAWorldCup #JFWorldCup2022
December 03, 2022
POLISI WASIPOTOA DHAMANA KWA MTUHUMIWA ANAWEZA KUWASHTAKI MAHAKAMANI - Mtuhumiwa aliyekamatwa na Polisi kama kosa lake linadhaminika na hajapelekwa Mahakamani ndani ya Muda uliowekwa Kisheria anaruhusiwa kuomba Dhamana yeye mwenyewe au kupitia wakili - Polisi wakigoma kumpa dhamana, anaweza kufungua kesi Mahakamani kuomba “Habeas Corpus,” ili Mahakama ilazimishe apelekwe Mahakamani kisha aombewe dhamana akiwa Mahakamani - Mtuhumiwa akifungua kesi ya kuzuiwa kupewa dhamana, washtakiwa ni Mkuu wa Kituo, Mkuu wa Polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) - #JFSheria #JamiiForums
December 03, 2022
#FIFAWORLDCUP2022: UHOLANZI YAINGIA ROBO FAINALI - Imefanikiwa kufika hatua hiyo baada ya kuifunga Marekani katika Mechi ya 16 Bora kwa Magoli 3-1 - Uholanzi sasa inasubiri mshindi wa Mechi kati ya #Argentina dhidi #Australia katika hatua inayofuata - #Qatar2022 #FIFAWorldCup #JFWorldCup2022
December 03, 2022
SIMBA YAIKAANGA COASTAL UNION, PHIRI AKIFUNGA MAWILI - Ushindi wa Magoli 3-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga umeifanya Simba ifikishe pointi 34 na kukaa kwenye usukani wa Ligi Kuu Bara - #Simba ambayo imefunga magoli 31 ikiwa ndio timu inayoongoza kwa kuwa na Magoli mengi katika Ligi msimu huu, imepata magoli kupitia kwa Moses Phiri aliyefunga mawili na Clatous Chama - Coastal imebaki na pointi 12 katika Michezo 14 ikiwa nafasi ya 13 kwenye msimamo - #JFSports #LigiKuu #JamiiForums
December 03, 2022
BRAZIL: HALI YA MWANASOKA MKONGWE PELÉ YABADILIKA, AWEKWA CHINI YA UANGALIZI MAALUMU - Ripoti kutoka vyanzo mbalimbali vikiwemo #DailyMail na #Reuters zinaeleza Edson Arantes do Nascimento maarufu Pelé yuko chini ya uangalizi maalumu baada ya Matibabu ya Moyo na Mionzi kutompa nafuu - Pelé mwenye Miaka 82 alikimbizwa Hospitali Novemba 29, 2022 akisumbuliwa na Uvimbe wa Tumbo, Moyo kushindwa kufanya kazi pamoja kumpunguzia maumivu ya Saratani ya Utumbo Mpana - Nyota huyo aliisaidia Brazil kushinda Kombe la Dunia mara 3 Miaka ya 1958, 1962 na 1970, na alifunga magoli 643 katika Mechi 659 za Klabu ya Santos, na aliifungia Brazil Magoli 77 katika Michezo 92. - #JamiiForums #JFSports
December 03, 2022
SHINYANGA: WAATHIRIKA WA TOPE LA MGODI WA ALMASI WADAI FIDIA - Wakazi wa Kata ya Mwaduilohumbo ambao Nyumba na Mashamba yao yalifunikwa na tope la Bwawa Mgodi wa Williamson Diamond kupasuka, wameiomba Serikali kuharakisha tathmini ya Uharibifu ili walipwe Fidia - Bwawa la Maji machafu la Mgodi wa Williamson Diamond lilipasuka Novemba 7, 2022 na tope kusambaa kwenye Makazi ya Watu ambapo Kaya zaidi ya 30 zenye Wakazi 145 ziliathiriwa - Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude, amewataka Wananchi hao kuwa wavumilivu wakati zoezi la tathmini likiendelea huku akiwataka kutoa taarifa sahihi. #JamiiForums #SocialJustice #Accountability
December 03, 2022
INDONESIA: BUNGE KUPITISHA SHERIA, WATAKAOFANYA NGONO KABLA YA NDOA KWENDA JELA - Sheria hiyo inatarajiwa kupitishwa Mwezi Desemba 2022 ambapo adhabu yake ni kifungo cha hadi Mwaka mmoja Gerezani - Ikipitishwa itawahusu raia wote wazawa na wageni. Pia, itaruhusu Wazazi wa Watu ambao hawajafunga Ndoa kuwaripoti Vijana wao kama wameshiriki Tendo hilo - Kuishi pamoja kabla ya Ndoa pia kutapigwa marufuku na wale watakaopatikana na hatia wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi Miezi sita jela - #Governance #JamiiForums
December 03, 2022
NIGERIA: MASHTAKA DHIDI YA MWANAFUNZI ALIYEMTUSI MKE WA RAIS YAFUTWA - Aminu Adamu (24) alikamatwa kutokana na ujumbe wa #Twitter ambapo alidaiwa kumtuhumu Mke wa Rais kwa kutumia vibaya Fedha za Umma na kushtakiwa kwa kueneza Habari za Uongo - Kukamatwa na mashtaka yaliyofuata dhidi ya Mwanafunzi huyo kulizua hasira huku watumiaji wengi wa Mitandao ya Kijamii na Wanaharakati wa Haki za Binadamu wakitaka aachiliwe mara moja - Shirika la Amnesty International limesema Mwanafunzi huyo aliteswa baada ya kukamatwa, na kukitaja kuwa kitendo cha ukandamizaji ambacho kinakiuka Haki za Kibinadamu, madai ambayo hadi sasa Mamlaka haijatoa Kauli yoyote. - #JamiiForums #HumanRights #Democracy #FreedomOfSpeech
December 03, 2022
Similar accounts
Disclaimer
The data provides is not authorized by TikTok. We are not an official partner of TikTok.
Use of materials from the resource is permitted only with a link to our resource.
Contact