aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi amevuka kihunzi cha kwanza katika mapambano ya kisheria ya mirathi baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali pingamizi dhidi ya maombi yake kuhusu wosia. Jacqueline amefungua maombi ya mapitio ya hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa Mei 18, 2021 na Jaji Yose Mlyambina iliyobatilisha wosia uliokuwa unadaiwa kuandikwa na marehemu Mengi wakati wa uhai wake, ambapo anaiomba Mahakama ya Rufani ifanye mapitio ya hukumu hiyo na hatimaye ibadilishe. #Bucket Proudly Sponsored By: #KIWINGU @goodtimezTZ @goodtimezTZ Ni mwisho wa siku na tuko na Kiwingu na tunakula Good times. Tafuta Kiwingu yako na ugonge cheers to the #SpiritOfGoodTimes #KiwinguSpirit #SpiritOfGoodTimes
October 13, 2021
Exclusive ndani ya @lavidaviwasafi LEO ! Tupo na De La Boss , Bugatti , Triple King ! Semaji La Dunia @hajismanara Kutoka Timu ya Wananchi . Leo anakuja kuzungumza Mapenzi 🤭!! Unatamani kufahamu nini kuhusu Maisha yake ya Mahusiano ? Drop Your Comments 👇🏽 @lavidaviwasafi with @divatheebawse ! Kuanzia Saa 4 Kamili Usiku on @wasafifm na YouTube | WASAFIMEDIA .
October 13, 2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio la kuchomwa moto baadhi ya nyaraka mbalimbali ambazo zilikuwemo ndani ya ofisi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Tunduma. #MenuYaLeo
October 13, 2021
Leo oct 13,202 Hopsitali ya Benjamini mkapa iliyopo jijini Dodoma imeadhimisha miaka 6 toka kuanzishwa kwake,katika sherehe ya maadhimisho hayo wafanyakazi wamesherekea pamoja na wagonjwa na kufanya zoezi la upandaji miti katika eneo la Hospitali hiyo. Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt Alphonce Chandika pamoja na Mganga mkuu wa macho Dkt Jucinta Feksi wanaeleza wapi walipofikia katika utoaji huduma toka kunzishwa kwa Hospitali hiyo. cc:@carlosngonya #WasafiDigital
October 13, 2021
Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Abdulrazak (mwenye asili ya Tanzania ) kwa kutunukiw tuzo ya Nobel prize na kumualika aje Zanzibar alipozaliwa. #MenuYaLeo
October 13, 2021
Mkazi mmoja wa kitongoji cha Ayatlaa kilichopo Kijiji cha Riroda kata ya Riroda wilayani Babati mkoani Manyara aliyefahamika kwa jina la Monica Nyaya (65) amejinyonga hadi kufa na mwili wake kukutwa ukining'inia juu ya mti Akizungumza na #wasafiFM mmoja wa familia ya marehemu amesema kuwa Monica Nyaya alitoweka nyumbani kwake tarehe 9 mwezi huu majira ya jioni huku akiaga kuwa anaenda kwa binti yake kusalimia na hakuonekana tena, wananchi walichukua jukumu la kumtafuta ndipo leo asubuhi wakamkuta katikati ya mlima wa Ayatlaa akining'inia juu ya kamba na kwa kuwa mwili wake umeharibikia familia imeamua kumzika hii leo Kwa upande wao viongozi wa eneo hilo wamesema kuwa baada ya kupata taarifa ya kupotea kwa mama huyo waliitana na kijiji kikaanza kumtafuta wakamkosa lakini walipomtafuta kwa mara ya pili ndipo wakakuta mwili umening'inia katikati ya mlima wa Ayatlaa kwa upande wake diwani wa kata hiyo amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa matuko ya aina hiyo katika kata hiyo wamekubaliana mtu yeyote atakayeonesha ishara ya kutaka kujiua au kutishia kunywa sumu watoe taarifa katika ofisi za vijiji au kituo cha polisi ili kupunguza matukio hayo #WasafiDigital
October 13, 2021
Exclusive Interview na @poshyqueeen kipindi cha #Mashamsham @wasafifm. Full interview @wasafifm na YouTube | WASAFIMEDIA
October 13, 2021
Leo Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki katika sala fupi ya kumuombea aliyekuwa Rais wa awamu ya 5, Hayati Daktari John Pombe Magufuli Wilayani Chato Mkoani Geita. #MenuYaLeo
October 13, 2021
DIAMOND ATUMIA MILIONI 69 KUNUNUA SAA / APEWA CARD HII . Superstar @diamondplatnumz ameendelea kuvunja Benki na Kununua Vito vya thamani , Baada ya Siku ya Leo Kununua saa aina ya @rolex yenye thamani ya Tsh. Milion 69 . Diamond amenunua saa hiyo nchini Marekani ambapo yupo Kwa ajili ya Tour yake ya Muziki , na Kupewa #InternationalWarrantyCard , ambayo inamuwezesha kupata Matengenezo ya saa hiyo sehemu yoyote ile Duniani . Je, wewe saa yako unayovaa Ina thamani ya Shilingi ngapi 😆 ? #HEADLINES with @abuusamii
October 13, 2021
Leo ni oct 13,2021 na tukiwa katika wiki ya siku ya maadhimisho ya afya ya macho duniani Wazazi wameshauriwa kuwaacha watoto wakacheze mtaani ili kuwaepusha na na matatizo ya macho, Hayo yamesemwa na Dkt Jucinta Feksi mganga mkuu wa macho kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari,Dkt Feks amesema kuwa kuwazuia watoto kwenda kucheza mitaani kunauwezekanao mkubwa wa kusababisha watoto hao kupata matizo ya kutokuona kwa sababu ya kukosa nafasi ya kuweza kuona mbali. "unajua zamani watoto walikuwa wanaenda kucheza kule mitaani mitaani,lakini siku hiziwatoto wapo wengi wa geti kali usitoke kaa ndani kwahiyo mara nyingi anakua anajua mimi natakiwa kuona vitu vya karibu tu"amesema Dkt.Jucinta Feksi Cc:@carlosngonya #WasafiDigital
October 13, 2021
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imepanga kuanzia Octoba 18 Mwaka huu kusikiliza mfululizo kwa Juma moja Kesi ya Uhujumu Uchumi na utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya na wenzake Sita. Hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha Dkt Patricia Kisinda Leo octoba 13 amatoa maamuzi hayo wakati kesi hiyo ilipokuja kwaajili ya kutajwa. Kesi hiyo namba 27/2021 ina Mashtaka matano ambapo matatu yanamkabilj Sabaya peke yake huku mawili yakimkabili na wenzake sita. Sabaya na wenzake inadaiwa mnamo January 22 mwaka huu maeneo ya jijini Arusha walitenda vitendo vya rushwa, na utakatishaji fedha kwa kujipatia kiasi cha shilingi milioni 90 kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mroso ili wasitoe taarifa za kodi aliyokiwa anadaiwa na serikali. Itakumbukwa kuwa katika kesi hii jamhuri imeshapeleka mashahidi watatu kati ya ishirini ambayo iliahidi itawapeleka mahakmani kwaajili ya ushahidi. Cc: @profit_Mmanga #WasafiDigit
October 13, 2021
Similar accounts
Disclaimer
The data provides is not authorized by TikTok. We are not an official partner of TikTok.
Use of materials from the resource is permitted only with a link to our resource.
Contact