@wasafifm

Wasafi FM

Tanzania
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imepanga kuanzia Octoba 18 Mwaka huu kusikiliza mfululizo kwa Juma moja Kesi ya Uhujumu Uchumi na utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya na wenzake Sita.

Hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha Dkt Patricia Kisinda Leo octoba 13 amatoa maamuzi hayo wakati kesi hiyo ilipokuja kwaajili ya kutajwa.

Kesi hiyo namba 27/2021 ina Mashtaka matano ambapo matatu yanamkabilj Sabaya peke yake huku mawili yakimkabili na wenzake sita.

Sabaya na wenzake inadaiwa mnamo January 22 mwaka huu maeneo ya jijini Arusha walitenda vitendo vya rushwa, na utakatishaji fedha kwa kujipatia kiasi cha shilingi milioni 90 kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mroso ili wasitoe taarifa za kodi aliyokiwa anadaiwa na serikali.

Itakumbukwa kuwa katika kesi hii jamhuri imeshapeleka mashahidi watatu kati ya ishirini ambayo iliahidi itawapeleka mahakmani kwaajili ya ushahidi.

Cc: @profit_Mmanga
#WasafiDigit

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imepanga kuanzia Octoba 18 Mwaka huu kusikiliza mfululizo kwa Juma moja Kesi ya Uhujumu Uchumi na utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya na wenzake Sita. Hakimu mkazi wa mahakama ya hakimu mkazi Arusha Dkt Patricia Kisinda Leo octoba 13 amatoa maamuzi hayo wakati kesi hiyo ilipokuja kwaajili ya kutajwa. Kesi hiyo namba 27/2021 ina Mashtaka matano ambapo matatu yanamkabilj Sabaya peke yake huku mawili yakimkabili na wenzake sita. Sabaya na wenzake inadaiwa mnamo January 22 mwaka huu maeneo ya jijini Arusha walitenda vitendo vya rushwa, na utakatishaji fedha kwa kujipatia kiasi cha shilingi milioni 90 kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mroso ili wasitoe taarifa za kodi aliyokiwa anadaiwa na serikali. Itakumbukwa kuwa katika kesi hii jamhuri imeshapeleka mashahidi watatu kati ya ishirini ambayo iliahidi itawapeleka mahakmani kwaajili ya ushahidi. Cc: @profit_Mmanga #WasafiDigit

October 13, 2021

Disclaimer

The data provides is not authorized by TikTok. We are not an official partner of TikTok.

Use of materials from the resource is permitted only with a link to our resource.

Copyright © 2024 insiflow.com