Mkazi mmoja wa kitongoji cha Ayatlaa kilichopo Kijiji cha Riroda kata ya Riroda wilayani Babati mkoani Manyara aliyefahamika kwa jina la Monica Nyaya (65) amejinyonga hadi kufa na mwili wake kukutwa ukining'inia juu ya mti Akizungumza na #wasafiFM mmoja wa familia ya marehemu amesema kuwa Monica Nyaya alitoweka nyumbani kwake tarehe 9 mwezi huu majira ya jioni huku akiaga kuwa anaenda kwa binti yake kusalimia na hakuonekana tena, wananchi walichukua jukumu la kumtafuta ndipo leo asubuhi wakamkuta katikati ya mlima wa Ayatlaa akining'inia juu ya kamba na kwa kuwa mwili wake umeharibikia familia imeamua kumzika hii leo Kwa upande wao viongozi wa eneo hilo wamesema kuwa baada ya kupata taarifa ya kupotea kwa mama huyo waliitana na kijiji kikaanza kumtafuta wakamkosa lakini walipomtafuta kwa mara ya pili ndipo wakakuta mwili umening'inia katikati ya mlima wa Ayatlaa kwa upande wake diwani wa kata hiyo amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa matuko ya aina hiyo katika kata hiyo wamekubaliana mtu yeyote atakayeonesha ishara ya kutaka kujiua au kutishia kunywa sumu watoe taarifa katika ofisi za vijiji au kituo cha polisi ili kupunguza matukio hayo #WasafiDigital
October 13, 2021
Disclaimer
The data provides is not authorized by TikTok. We are not an official partner of TikTok.
Use of materials from the resource is permitted only with a link to our resource.
Contact