@albertomsando

Advocate Albert G. Msando

Unknown

Instagram posts and videos uploaded by albertomsando

albertomsando

class="content__text"

March 05, 2023

albertomsando

class="content__text" #PleaseSwipe. Leo ni siku ya nne kuendelea na kambi ya kusikiliza [kuishi] na wananchi hapa Kiji cha Msomera. Tumeendelea kutoa huduma lakini kubwa tumeweza kusikia mawazo na maoni yao kuhusu masuala mengi ambayo tukiyafanya kwa pamoja tutafanikiwa sana. Tumekubaliana hata siku ya wanawake tarehe 8/03 tutaadhimisha hapa kwa kusheherekea mila na desturi zetu makabila yote tulio hapa. Leo tunaendelea na mazungumzo kupokea ushauri wa viongozi wa mila na dini. Tunakumbuka kwamba hatujui sana kuliko wao. Kufahamu kwetu sio kujua zaidi. Tutajua tukisikiliza na kuelewa wanachofahamu wao. #Jumapili #Kambini #MsomeraTobiko #SSHKazini

March 05, 2023

albertomsando

class="content__text" Uwezeshaji makundi maalumu kiuchumi Wilaya ya Handeni. Halmashauri za Handeni Mji (Handeni Township Council) na Wilaya ya Handeni (Handeni District Council) zimetoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Nawapongeza watendaji wote pamoja na Wahe. Madiwani kwa kutekeleza sheria. #Swipe #Glass-gow

March 04, 2023

albertomsando

class="content__text" PART TWO: Amidst all key drivers of change lies the most potent driver, which is climate change (Jandreau & Berkes, 2016). It reduces the land area suitable for traditional pastoralist lifestyle, erodes the relationship between the Maasai and their historical territories (Ahmed et al, 2014) and is responsible for induced natural disasters (Ruppel, 2013) such as floods and prolonged draughts. The Maasai have therefore been forced to abandon their traditional nomadic lifestyles to survive. Their [animal] freedom of movement in search of water and pasture is restricted. They must now reduce the number of their cattle to avoid ‘overgrazing’. They can no longer proudly feed solely on milk, meat and blood instead they have to supplement with agricultural products and even fish which was taboo for them. And so we must do a soul-searching exercise as we are strategizing how to survive as a group [the modern Maasai]. The reality is painfully clear. And there is hardly a way out except adaptation, which actually has been the only way out time immemorial. And mitigation? 🤷🏿‍♂️ Written by, Adv. Albert G. Msando 2023. NB: Andiko hili ni sehemu ya notes zangu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na athari kwa mila, desturi na tamaduni. @binamubananga samahani sana. Next time. 🙏🏿

March 04, 2023

albertomsando

class="content__text" **Extracts of My Thoughts** PART ONE: Human culture, a social phenomenon is a subject of change. Pastoralism is a culture that represents the traditional Maasai and identifies them as a tribe. Their relationship with, and ownership of cattle has proprietary and sentimental value. For the Maasai man, the number of children and cattle, which are considered as a currency, are measures of wealth and social status (Ahmed et al, 2014, Briggs, 2006).   However, it is well documented that the Maasai pastoralists are changing (Coast 2002; Thompson 2002; Worden 2007; Sachedina 2008; BurnSilver 2009; Galvin 2009; Nkedianye et al. 2009; Reid et al. 2014). The future of pastoralism, which is the defining cultural practice of the nomadic Maasai, is precarious (Prins 1992). What are we doing about it? #ReadNext #Continuing

March 04, 2023

albertomsando

class="content__text" Tunapotaka kufika ni mbali. Hatuwezi kupaona kwa macho. Ila kwa fikra chanya, uthubutu na utayari wa kutenda kwa kuamini tutafika na kupaona. Changamoto zetu ni fursa. #Handeni #TazamaIliUone

March 04, 2023

albertomsando

class="content__text" #KwamaiziHandeni. Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Maji @wizarayamajitz ilileta mitambo ya kuchimba Bwawa la Kwenkambala tarehe 3 na 6 mwezi wa pili mwaka huu. Baada ya kupokea mitambo hiyo sisi kama Wilaya tumejiongeza na kuomba ridhaa tuchimbe na Bwawa la Kwamaizi ambalo usanifu wake ulishafanyika huko nyuma. Ombi letu limekubaliwa na jana kazi hiyo imeanza Bwana la Kwamaizi. Tumejiongeza kugawanya mitambo sehemu zote mbili kupishanisha kazi. Tunapasua miamba Kwenkambala na kuchimba na tunasafisha eneo na kuanza uchimbaji Kwamaizi. Kizigua inaitwa two in one. Hatutalala mpaka tuyakamilishe yote kwa wakati. Mabwawa haya yatapunguza kwa kiasi kikubwa kero ya maji Handeni mjini Kata ya Chanika na kata nyingine za jirani. Nampongeza sana Mhe. Kagwilwa (Mamba), Mbunge wa Handeni Mjini, kwa kufuatilia miradi hii. Amepambana sana. Pia Mhe. Diwani Kata ya Chanika na Afisa Tarafa Chanika kwa kusimamia miradi yote kila siku. Nawapongeza sana. Niwaombe wananchi wa Handeni waendelee kuwa wavumilivu. Kilio kuhusu maji Serikali inakifanyia kazi. Muda si mrefu tutaimaliza kabisa kero hii au itapungua kwa kiasi kikubwa. Serikali ipo kazini. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kumtua mama ndoo kichwani. ANATEKELEZA AHADI KWA VITENDO. #MajiHandeni @jumaa_aweso@gipson_george

March 03, 2023

albertomsando

class="content__text" Mojawapo ya changamoto ya jumla tuliyokutana nayo ni upungufu wa chakula msimu huu. Hali ya ukame imetuathiri wilaya ya Handeni. Pamoja na utabiri wa hali ya hewa ni muhimu kuwa karibu sana na wananchi kushauriana nini cha kupanda. Endapo tutapanda kwa kutegemea ‘kudra’ za Mwenyezi Mungu pekee tutapata hasara. Mazao yanayohimili ukame kama Mtama na Mihogo yatatusaidia. #Handeni #Kilimo #TabiaNchi Nb: Nikiwa na Mwenyekiti na Mtendaji wa Kijiji. Familia ya kazi ya kuwahudumia wananchi.

March 03, 2023

albertomsando

class="content__text" #Msomera. Siku ya kwanza. Tumesikiliza na kutatua changamoto. Kesho tunaendelea. Huduma mbalimbali kama NIDA, Bima ya Afya, Usajili TASAF, Ardhi, Vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5, Usajili wa Vikundi, TIN nk zimeanza kutolewa. Tutaendelea mpaka tarehe 11. Ila tutahakikisha hii inakuwa endelevu kuwarahisishia wananchi na pia kuongeza mapato kwa Serikali kutokana na ada mbalimbali zitakazolipwa. Tutaboresha namna ya utoaji huduma (Mobile Service Provision). #MsomeraTobiko @handenidc355

March 03, 2023

albertomsando

class="content__text" Mara ngapi asubuhi saa 12 jirani yako anakuja kukusalimia na kunywa chai pamoja? Mapema kabisa hapa kijiji cha Msomera Mwenyekiti wa Kijiji amekuja tunywe kahawa. Na kuendelea kuzungumza kuhusu wananchi wake. #SSHKazini. KARIBUNI MSOMERA MUONE KAZI KUBWA INAYOFANYWA NA SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WANANCHI WALIOHAMIA KWA HIARI KUTOKA NGORONGORO NA WALIOKUWA HAPA. EPUKA UPOTOSHAJI. Tuko site.

March 02, 2023

albertomsando

class="content__text" Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga madarasa mawili ya TEHAMA kwenye shule ya Msingi ya Samia Suluhu na shule ya Sekondari Msomera kwa gharama ya Milioni 179. Tumepokea mradi huu uliokabidhiwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Kazi inaendelea. #SSHKazini

March 02, 2023

albertomsando

class="content__text" #MsomeraTobiko. Nimetembelewa na wazee wa Kijiji cha Msomera. Tumechoma nyama ‘kiasili’ kwa mlo wa jioni. Tukiwa chini ya mti tumefungua milango ya kuanza kazi hapa mpaka tarehe 12/03/2023. Lengo ni, 1. Huduma kuwafikia wananchi walipo badala ya wao kuifuata kwa gharama ya muda na nauli 2. Kushuka walipo wananchi na kutatua changamoto kwa kuona uhalisia 3. Kufurahi na wananchi kwa sababu wote ni wananchi. Wanadamu wote ni sawa. Ahadi ya MwanaCCM. Ilianzia TANU. Karibuni sana Msomera. Kijiji cha mfano. #karibuni

March 02, 2023

Similar accounts

natgeo

284.3m followers

@natgeo
iamcardib

169.3m followers

@iamcardib
ddlovato

157.4m followers

@ddlovato
realmadrid

152.8m followers

@realmadrid
chrisbrownofficial

145.3m followers

@chrisbrownofficial
fcbarcelona

125.6m followers

@fcbarcelona
championsleague

113.4m followers

@championsleague
gal_gadot

109.3m followers

@gal_gadot
sooyaaa__

77.4m followers

@sooyaaa__
premierleague

72.7m followers

@premierleague
theweeknd

71.7m followers

@theweeknd
urvashirautela

70.3m followers

@urvashirautela

Disclaimer

The data provides is not authorized by TikTok. We are not an official partner of TikTok.

Use of materials from the resource is permitted only with a link to our resource.

Copyright © 2024 insiflow.com