@voaswahili

VOA Swahili

Unknown

Instagram posts and videos uploaded by voaswahili

voaswahili

class="content__text" Mtoto wa KIke Azaliwa Ndani ya Kifusi Cha Tetemeko la Ardhi Wananchi wanaoendelea kuchimba kifusi cha jengo lililoanguka katika mji wa kaskazini magharibi mwa Syria wamegundua mtoto analia ambaye mama yake inaelekea alimzaa wakati akiwa amefunikwa na kifusi katika tetemeko la ardhi lililotokea wiki hii lililoketa uharibifu mkubwa.
 Kitovu cha mtoto huyo aliyezaliwa kilikuwa bado kimeungana na mama yake, Afraa Abu Hadiya, ambaye alifariki, wamesema.
 Mtoto huyu ndiye mwanafamilia pekee aliyenusurika jengo lilipoporomoka Jumatatu katika mji mdogo wa Jinderis, likiwa karibu na mpaka wa Uturuki, Ramadan Sleiman, ndugu wa familia, ameliambia shirika la habari la AP.   Tetemeko la ardhi lilitokea kabla ya alfajiri lenye ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha rikta, lililofuatiwa na matetemeko madogo madogo, yaliyo sababisha uharibifu eneo lote la upande wa kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria. ( Chanzo cha habari ni shirika la habari la AP). #usmilitary #china #reels #videography #voiceofamerica #voa #voaswahili #swahili #africa #afrika #afirka #marekani🇺🇸 #syria #turkey #earthquake #miracle

February 14, 2023

voaswahili

class="content__text" Watu zaidi waokolewa kutoka katika vifusi Ijumaa katika sehemu mbalimbali za Uturuki. Mmoja wa manusura alipatikana chini ya kifusi baada ya saa 100. Ungana na mwandishi wetu kwa ripoti kamili #uturuki #syria #tetemekolaardhi #dunianileo #voa #voaswahili #uokoaji #miili #manusura

February 11, 2023

voaswahili

class="content__text" Wanafunzi wamelazimika kusomea katika kituo cha treni kilichopo chini ya ardhi mjini Kyiv, kufuatia mashambulizi mapya ya makombora. #wanafunzi #russia #mashambulizi #ukraine. #kyiv #vituovyatreni #voa #voaswahili #dunianileo

February 11, 2023

voaswahili

class="content__text" Kiongozi wa Korea Kaskazini na binti yake washiriki katika gwaride kubwa la kijeshi mjini Pyongyang Jumatano. Katika muhtasari wa ripoti hii mwandishi wetu anakuletea yale ambayo yanazungumziwa kuhusu kiongozi huyu na binti yake. Pia utaweza kufahamu ni matayarisho gani Korea Kaskazini inafanya kati Rasi ya Korea. #koreakaskazini #pyongyang #gwaride #jeshi #silaha #voa #voaswahili #dunianileo

February 10, 2023

voaswahili

class="content__text" Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameendelea na ziara yake nchini Marekani Jumatano huko Wizara ya Ulinzi ya Marekani- Pentagon ambako alikutana na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin. Viongozi hao wamejadili mambo kadhaa. Sikiliza muhtasari wa ripoti hii maalum anayokuletea mwandishi wetu Mkamiti Kibayasi... #katibumkuu #nato #jensstoltenberg #ziara #marekani #waziriwaulinzi #lloydaustin #ukraine #uvamiziwarussia #voa #voaswahili #dunianileo

February 10, 2023

voaswahili

class="content__text" Ungana nami Mary Mgawe katika matangazo ya Duniani Leo kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika...

February 10, 2023

voaswahili

class="content__text" Marekani yatungua Puto la China lililoshukiwa kufanya Ujasusi Puto la China laanguka kutoka angani baada ya kupigwa na kombora
 Marekani imelitungua puto la China lililoshukiwa kufanya ujasusi likiwa linaelea kuelekea pwani ya kusini mashariki mwa Marekani Jumamosi, maafisa wa Marekani walisema.
 Macho yalikuwa yameelekezwa angani Jumamosi wakati puto la China linaloshukiwa kufanya ujasusi lilipopita eneo la mpaka wa baharini mashariki mwa Marekani – ambako mamlaka za eneo ziliwatadharisha raia dhidi ya kutungua puto bila ya njia ya kujihami, wakitumia bunduki zao – kabla ya kutunguliwa lilipokuwa limeingia katika Bahari ya Atlantiki.
 Lilitunguliwa na kuangushwa nje ya pwani ya California Jumamosi mchana na operesheni ilianzishwa kukusanya mabaki ya puto hilo. Utawala wa Biden kabla ya hapo ulisita kulitungua puto hilo kwa sababu ya kutohatarisha maisha ya watu walioko nchi kavu kutokana vipande vya puto vitakavyoanguka likitunguliwa.
 Puto hilo lenye kusogea liliingia anga ya Marekani kutoka Alaska mapema wiki hii na maafisa wa serikali hawakuwa wamethibitisha hilo mpaka Alhamisi, siku moja baada ya ndege za biashara zilipositisha kwa muda safari zake katika uwanja wa ndege huko Billings, Montana na watu waliokuwa ardhini kulishuhudia puto hilo likielea juu ya anga ya mji huo.
 China ilisema ilikuwa ni chombo cha kutafiti hali ya hewa kilichopeperushwa nje ya eneo lilikotakiwa kuwa, madai yaliyotupiliwa mbali na maafisa wa Marekani waliosema chombo hicho kilikuwa kimepita maeneo kadhaa ya Montana ambako makombora ya nyuklia yanahifadhiwa. #usmilitary #china #reels #videography #beijing #voiceofamerica #voa #voaswahili #swahili #africa #afrika #afirka #marekani🇺🇸 #chineseballoon

February 09, 2023

voaswahili

class="content__text" Hatua ya Marekani kulitungua puto linalodaiwa kuwa la kijasusi likiwa angani kwenye Bahari ya Atlantic, nje ya pwani ya South Carolina. Lakini nini ambacho China imeeleza kuhusu kadhia hiyo ya kutunguliwa puto lao. Endelea kusikiliza kwa muhtasari jibu la China... #marekani #puto #ujasusi #bahariyaatlantic #southcarolina #china #voa #voaswahili #dunianileo

February 09, 2023

voaswahili

class="content__text" Rais Joe Biden akilieleza nia yake ya dhati kufanya kazi na China akiweka wazi kile ambacho kinaweza kufanya dhamiri hiyo isifikiwe. Endelea kusikiliza Rais akieleza kuwa tayari Marekani imeonyesha mfano kwamba pale China ilipotishia usalama wa Marekani imechukua hatua.... #rais #joebiden #china #ushirikiano #marekani #puto #ujasusi #voa #voaswahili #dunianileo

February 09, 2023

voaswahili

class="content__text" Rais wa Marekani Joe Biden aeleza: Hivi leo tuna nguvu zaidi kwa miongo kadhaa na tunaweza kushindana na China na yeyote yule ulimwenguni. Na naahidi... Naahidi kufanya kazi na China ambapo tunaweza kuendeleza maslahi ya Marekani na kuunufaisha ulimwengu, lakini usijidanganye kuhusu hilo, kama tulivyoweka wazi wiki iliyopita, iwapo China itatishia uhuru wetu tutachukua hatua kulinda nchi yetu na tumefanya hivyo. ... #rais #marekani #joebiden #china #ushindani #ulimwengu #maslahi #uhuru #hotuba #haliyakitaifa #voa #voaswahili #dunianileo

February 08, 2023

voaswahili

class="content__text" Madaktari wanasema asilimia 17 ya wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa katika vita vya uvamizi wa Russia nchini Ukraine wanamajeraha yanayohitaji matibabu ya hali ya juu. Endelea kusikiliza ni kinafanyika kukabiliana na hali hiyo na ni wapi wanajeshi hao wanatarajiwa kupatiwa matibabu.... #madaktari #matibabu #Ukraine #wanajeshi #vita #uvamiziwarussia #voa #dunianileo #voaswahili

February 08, 2023

voaswahili

class="content__text" "Rais wa Marekani katika hotuba yake ya Hali ya Kitaifa Jumanne usiku akihutubia bunge la Marekani anasema: "Mafanikio yetu siyo mfano wa nguvu zetu, ni nguvu ya mfano wetu. Tukumbuke dunia inatuangalia ..." #rais #marekani #hotuba #haliyakitaifa #bungelacongress #marekani #umoja #voa #voaswahili #dunianileo

February 08, 2023

Similar accounts

natgeo

284.3m followers

@natgeo
iamcardib

169.3m followers

@iamcardib
ddlovato

157.4m followers

@ddlovato
realmadrid

152.8m followers

@realmadrid
chrisbrownofficial

145.3m followers

@chrisbrownofficial
fcbarcelona

125.6m followers

@fcbarcelona
championsleague

113.4m followers

@championsleague
gal_gadot

109.3m followers

@gal_gadot
aliaabhatt

84.6m followers

@aliaabhatt
sooyaaa__

77.4m followers

@sooyaaa__
karimbenzema

76.5m followers

@karimbenzema
premierleague

72.7m followers

@premierleague

Disclaimer

The data provides is not authorized by TikTok. We are not an official partner of TikTok.

Use of materials from the resource is permitted only with a link to our resource.

Copyright © 2024 insiflow.com