class="content__text" Mtoto wa KIke Azaliwa Ndani ya Kifusi Cha Tetemeko la Ardhi Wananchi wanaoendelea kuchimba kifusi cha jengo lililoanguka katika mji wa kaskazini magharibi mwa Syria wamegundua mtoto analia ambaye mama yake inaelekea alimzaa wakati akiwa amefunikwa na kifusi katika tetemeko la ardhi lililotokea wiki hii lililoketa uharibifu mkubwa. Kitovu cha mtoto huyo aliyezaliwa kilikuwa bado kimeungana na mama yake, Afraa Abu Hadiya, ambaye alifariki, wamesema. Mtoto huyu ndiye mwanafamilia pekee aliyenusurika jengo lilipoporomoka Jumatatu katika mji mdogo wa Jinderis, likiwa karibu na mpaka wa Uturuki, Ramadan Sleiman, ndugu wa familia, ameliambia shirika la habari la AP. Tetemeko la ardhi lilitokea kabla ya alfajiri lenye ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha rikta, lililofuatiwa na matetemeko madogo madogo, yaliyo sababisha uharibifu eneo lote la upande wa kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria. ( Chanzo cha habari ni shirika la habari la AP). #usmilitary #china #reels #videography #voiceofamerica #voa #voaswahili #swahili #africa #afrika #afirka #marekani🇺🇸 #syria #turkey #earthquake #miracle
February 14, 2023
Disclaimer
The data provides is not authorized by TikTok. We are not an official partner of TikTok.
Use of materials from the resource is permitted only with a link to our resource.
Contact